Tuesday, September 4, 2012

Waziri Nchimbi Amshangaa IGP, Kwa nini mpaka sasa hajamkamata Dr. Slaa



Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi ameelezea kushangazwa kwake na ukimya wa mkuu wa jeshi la polisi nchini juu ya sakata la kuuwawa kwa mwandishi wa habari mkoani Iringa.
Waziri Nchimbi amedai kuwa siku moja kabla ya Chadema kufanya mikutano na ufunguzi wa ofisi za chama wilayani Mufindi Dr. Slaa alimtumia ‘sms’ mkuu huyo wa jeshi la polisi nchini akimtaka ampigie simu haraka pia vinginevyo aandae risasi za kutosha kwa ajili ya kuwaua kwani hawangekuwa tayari kuvumilia uonevu na ukandamizaji unaofanywa na jeshi lake.
Waziri Nchimbi anadai kitendo cha IGP kuendelea kukaa kimya bila kutoa tamko lolote kufuatia kifo cha Mwangosi siku moja baada ya kupokea ‘sms’ toka kwa Dr. Slaa, na kitendo cha jeshi la polisi kushindwa kumkamata Dr. Slaa kinamuonyesha kwamba yeye (IGP) ni dhaifu sana, ama hajui wajibu wake, na iwapo huko mbeleni Dr. Slaa atakuwa raisi wa nchi atampuuza na kumdharau sana.

No comments:

Post a Comment