Saturday, October 6, 2012

Rick Ross Amewasili Dar es Salaam

 Meneja wa Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012, Allan Chonjo akisalimiana na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Rick Ross mara baada ya kuwasili usiku wa Ijumaa, Oktoba 5, 2012 nndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius K. Nyerere, akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzake pichani nyuma. Waliop kati ni Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd, Balozi Kindamba ambao ndio waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalotarajiwa kufanyika hapo Jumamosi, Oktoba 6, 2012.
 
Rick Ross akitoa salamu ya salut kwa washabiki wake waliojitokeza usiku huu (hawapo pichani) kumlaki
Operesheni Meneja wa Prime Time Promotions, Balozi Kindamba akiwaongoza wageni wake kuelekea kwenye gari tayari kuondoka kuolekea kwenye hoteli waliopangiwa kufikia usiku huu. Kuhoto ni Rick Ross na akiwa na baadhi wanamuziki wenzake aliombatana nao.
Rick Ross akiingia ndani ya mchuma.
Rick Ross akiondoka na mchuma wake kuelekea hotelini, Oktoba 5, 2012 usiku.
Mmoja wa mashabiki wa Rick Ross aliyezua tafrani kiaina akijifananisha na Rick Ross akizungumza na na baadhi ya watu waliojitokeza kumlaki The Big Boss mwenye Rick Ross.

Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA Arusha: Watuhumiwa watoroka mahakamani mbele ya polisi!


Vyanzo zaidi vimeweza kutupatia ukweli wa hasa kilichojiri leo mahakamani pale Arusha.
Watuhumiwa wawili wa mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo, aliyechinjwa kwa kitu kikali mithili ya msumeno, wametoroka mahakamani leo Arusha, mbele ya askari polisi. Itakumbukwa hii kesi inahusisha viongozi aw CCM.
Kama kuonesha kuwa video ya mpango huo isingenoga sana, watuhumiwa hao inasemekana wamemnyang’anya bunduki mmoja wa askari kati ya wengi waliokuwa wakiwalinda. According to the source, Askari waliokuwepo wakishuhudia saga hiyo, wakanogesha zaidi picha kwa kutochukua hatua yoyote, achilia mbali kulinda mali ya jeshi na serikali, hawakumsaidia hata mwenzao wakati anashambuliwa, kunyang’anywa bunduki na kuchaniwa nguo zake, call them uniform.
If that not enough to end the show, bunduki hiyo, according to source, iliokotwa muda mfupi baade ikiwa imetelekezwa. Another game in the making. Wanafikiri wananchi wrote wamelewa banana.
MORE INFO
And the beat if not the show goes on…baadhi ya maaskari waliokuwa ‘lindo’ wanashikiliwa polisi. Kesho kuna mahafali/shughuli pale CCP, kwa hiyo wakubwa pia wa hawa jamaa wako kwenye mji wa utalii.
Taarifa hii iliwekwa na Tumaini Makene Afisa Habari wa CHADEMA kama TETESI lakini imethibitishwa Bofya HAPA  kwa mjadala zaidi

Radi Inauzwa Sumbawanga Kwa bei Chee! Elfu Arobaini tu!


Na: Florence Majani,MWANANCHI
KWA wakazi wa Dar es Salaam, mawingu yanapotanda angani na kutengeneza giza ambalo huashiria mvua, kwao huwa ni jambo la kawaida na pengine ni ahueni kwa karaha za joto kali. Lakini kwa wakazi wa mkoa wa Rukwa, ikiwemo hasa Sumbawanga, dalili ya mvua inayoambatana na radi ni tishio la umauti, kwani mara nyingi radi hizi si za kawaida au za asili bali ni za kichawi na hutengenezwa na wanadamu kwa madhumuni ya kuua.
Mkoa wa Rukwa hususani wilaya ya Sumbawanga, ni eneo linalosifika kwa imani za kishirikina nchini. Lakini katika masuala ya utaalamu wa radi, yapo maeneo na watu maalum ambao wana uwezo wa kutengeneza radi. Ukiwa unatokea wilaya ya Sumbawanga kuelekea wilaya ya Nkasi, ndipo vilipo vijiji maarufu kwa kutengeneza radi hizo.
Baadhi ya vijiji hivyo ni Sintale na Chipu, ambako ndiko walipo wataalamu wenye uwezo na nguvu za ziada za kutengeneza radi. Kwa nini radi zinatengenezwa? Radi hizi zinatengenezwa kwa ajili ya kuua au kuwajeruhi maadui. Kwa mfano, kama yupo aliyekudhulumu, aliyekuibia mke au mume, aliyekugonga na gari bila kukulipia gharama za matibabu au anayekutusi na kukukebehi. Vijiji vya Sintale, Chipu na Kalundi, vimepakana, kinaanza kijiji cha Kalundi kisha Sintale na cha mwisho ni Chipu. Vijiji hivyo viko duni kimaendeleo na ukubwa.
Hata hivyo huku ndipo walipo watalaamu na mafundi wa kuunda radi. Nilipokuwa mkoani humo hivi karibuni na mwenyeji wangu, tulielekezwa na wenyeji wa Kalundi kwa mganga wa kwanza nayeitwa Mashaka ambaye anaaminiwa kwa kuunda radi. Baada ya kufika kwa Mashaka, tunamkuta akiwa na wateja kadhaa. Ninamweleza shida yangu na kumtonya kuwa ni shida ya kipekee kidogo. Namweleza kuwa nahitaji kununua radi kwani nina adui yangu aliyenidhulumu fedha nyingi. Mashaka anajibu kuwa yeye si mtaalamu wa radi bali anatibu maradhi tu.
Anasema: “Lakini yupo mtaalamu wa radi, anaitwa mzee Chimwaga, anaishi kijiji cha Sintale. Ngoja nimpigie simu sasa hivi,” Mganga huyu anazungumza kwenye simu kwa lugha ya kifipa, na baada ya dakika chache anakata simu na kutugeukia na kusema: “Yupo- nendeni- kutoka hapa kwenda Sintale kwa Honda ni dakika 20, mkimuuliza yeyote, atawapeleka kwa mzee huyo,” Kwa kuhofia muda, hatukwenda kwa mganga Mzee Chimwaga, na badala yake tunakwenda eneo jingine na kuuliza iwapo kuna mganga mwingine mwenye utaalamu wa radi. Mzee mmoja anatuelekeza kuwa yupo mganga anayeitwa Ntoro, mwenyeji wa hapo hapo Kalundi ambaye naye ni mtaalamu wa radi.
Tunaelekezwa kwa mganga Ntoro, tunapofika tunamkuta akiwa na wake zake wawili na watoto wasiopungua wanane. Anatukaribisha na tunamweleza shida yetu. Mganga Ntoro anasema, yeye hutengeneza radi lakini kwa wakati ule alikuwa kaishiwa vifaa, hivyo aliamua kumpigia simu mganga mwenzake mwenyeji wa kijiji cha Sintale ambaye ana ujuzi huo pia.
Anashika simu, na kumpigia mganga huyo tuliyebaini kuwa anaitwa Maisha, huku akimsisitizia afike haraka azungumze na wateja. Wakati tukimsubiri Mganga Maisha afike, tulianza kumdodosa Mganga Ntoro kuhusu utaalamu huo wa kuunda radi. Ntoro anasema, kwa kawaida huduma ya radi huuzwa, au hutozwa gharama kwa bei ya kuanzia Sh40,000 hadi 30,000 tu na hiyo ni kulingana na umbali wa eneo alipo mtu anayetakiwa kuuwawa na aina ya radi.
“Kwa mfano watu wanaotoka Zambia au Kongo tunawachaji fedha nyingi zaidi kwa sababu ya umbali, lakini kwa maeneo ya karibu bei ni nafuu kidogo,” anasema Ntoro. Radi hutengenezwaje? Ntoro anasema, kwa kabila la kifipa, utaalam wa kuunda radi huitwa ‘Namasata’. Radi hutengenezwa kichawi, lakini mtu yeyote anaweza kufundishwa na kuweza kuitengeneza, ili mradi afuate masharti. Anasema zipo radi za aina tatu, ya kwanza ni ya maji, ya pili ni ya pembe, na ya tatu ni ya gome la mti. Zote hizo hutengenezwa kulingana na umbali na ubora wake.
“Radi ya pembe ni ya hatari zaidi, huchoma na kuweza kutekeza watu na mali, na huenda umbali mrefu tofauti na radi ya gome la miti,” anasema Huku tukiendelea kumdadisi, mganga Ntoro anasema, radi ya maji hutengenezwa kwa kuchukua sahani mpya, bakuli mpya au chupa ya udongo. Kisha mtaalamu huweka dawa ndani ya chupa au bakuli na kuisemea maneno fulani.
“Ukishanuiza, unaviweka vifaa hivyo ndani, kesho asubuhi utakuta maji ndani ya chupa au kama uliweka bakuli basi utaona maji ndani ya bakuli,” anasema na kuongeza, “Baada ya hapo unachukua vifaa vile na kuanza kunuiza adhabu unayotaka impate mbaya wako, kwa kumtaja jina. Kama huna jina basi uwe na nyayo zake, nguo au kitu chake chochote kile.”
Anasema baada ya kunuiza, unachukua bakuli au chupa ikiwa juu ya sahani na kuyarusha maji yale juu, kwa nguvu za kichawi, maji yale hupotea lakini kama kutakuwa na kasoro yeyote, maji yale humrudia aliyeyarusha. Endapo mtaalamu atairusha radi ile kwa mtu asiye na makosa, basi maji yatarudi chini na kama kweli mtu yule amefanya kosa, basi maji hayatarudi na yatakwenda angani na kuanza kutengeneza wingu jeusi linaloambatana na ngurumo.
“Maji yakisharushwa juu, baada ya saa moja tu, utaanza kuona angani kiwingu cheusi na kizito sana, mvua inaweza kunyesha kidogo na kisha ngurumo za kutisha … basi hapo ujue kazi tayari na mbaya wako kashamalizwa,” anasema na kuongeza: “Kama unairusha radi kwa mtu asiye na makosa kabisa, au ukakosea masharti radi inaweza kukurudia na kukuunguza wewe.
Mtu akiniudhi mimi huwa nazirusha tu,” Radi ya pembe hutengenezwaje? Wakati tukiendelea kumsubiri mganga Maisha, kutoka Chipu, Mganga Ntoro anaendelea kutupa utaalamu huo bila kujua kuwa alikuwa akichunguzwa. Sasa anasimulia namna ya kutengeneza radi ya pembe. Anasema, radi hii hutengenezwa kwa pembe ya mbuzi au kondoo, ambayo kwa kawaida huwa na uwazi katikati.
‘Tunachukua pembe, tunaweka dawa ndani yake, (yaani kwenye uwazi) tunafunga hirizi kuizunguka pembe, pamoja na shanga, kisha tunanuiza maneno kadhaa ya kichawi, na kisha tunairusha kuelekea alipo mlengwa,” anasema Radi hii ni kama kimondo, inaporushwa, hupaa angani na hufuka moshi katika upande wa mbele wa pembe wenye uwazi kama zifanyavyo ndege za kushambulia(rocket). Mganga Ntoro anasema, radi hii huweza kupaa umbali mrefu na huweza kuharibu mali, mifugo na binadamu ambaye anawindwa.
Kuhusu namna ya kutengenez radi ya gome la mti, Ntoro anasema hiyo ina masharti makali ambayo si rahisi kuzitoa siri zake kwa kila mtu. Hata hivyo, baada ya muda mfupi, mganga Maisha anapiga simu na kusema kuwa ameshindwa kufika kwa sababu ametingwa na shughuli za mazishi na kutaka twende siku inayofuata asubuhi na mapema.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho, David Ntare anasema mauaji ya radi ni jambo la muda mrefu mahali hapo kwani wanaotumia uchawi wa radi wamekuwa wakijigamba mitaani kwa uweza wao huo. “Tangu nazaliwa nasikia vifo vya radi na nina uhakika si radi za kawaida kwa sababu, wanaokufa mara nyingi huwa na uhasama na mtu, kama kumuibia mke,mume, kuiba au kutukana,” anasema Ntare.
Ntare analihusisha tukio la kuungua kwa benki ya NMB, wilayani Nkasi, tarafa ya Namanyere lililotokea miaka ya nyuma na uchawi wa radi. “Ile benki iliunguzwa na radi na mzee mmoja mkulima wa kijiji cha Kizi baada ya aliibiwa hela nyingi katika akaunti yake, akaona alipe kisasi kwa njia ile. Ile benki iliungua wa radi, hakuna asiyejua,” anasema Inadaiwa kuwa wenyeji wa hapa aghalabu huviona vitu hivi na hujua madhumuni yake na mara nyingi vifo vya aina hii hutokea wilayani Sumbawanga. Anasema, kwa kawaida mtu aliyeungua kwa radi huwa kama aliyeungua kwa umeme.
“Huungua na kuwa weusi kama mkaa, na wakati mwingine radi hukataa kumuua mtu akiwa ndani, bali humrusha nje na kumchoma huko ili isiwadhuru watu wengine,” anasema. Mwalimu wa shule ya msingi Chalantala, Abeid Kisanga, anasema siku moja akiwafundisha wanafunzi wa darasa la tatu somo la sayansi kuhusu radi , mwanafunzi wa kiume alinyoosha kidole na kusema ‘mimi najua kutengeneza radi, baba kanifundisha,”
Anjelo Singo, Afisa wa Polisi tarafa ya Namanyere anasema suala la ushirikina wilaya ya Sumbawanga na Nkasi ni kubwa na yamekuwapo matukio kadhaa ya vifo vinavyodaiwa kusababishwa na imani hizo. “Ingawa serikali haiamini uchawi, lakini matukio ya radi yanayotokea hapa mengi ni ya kishirikina, au matukio ya watu kuuwawa na kukatwa sehemu za siri vilevile ni ya kishirikina,” anasema Anasema ni ukweli usiopingika kuwa uchawi umesheheni katika maeneo haya na wakazi wake wameshaathirika kisaiolojia kuhusu hilo.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya anasema ameshawahi kusikia taarifa za kuwepo kwa wataalamu wa kuunda radi lakini akasema hata hivyo hana uhakika nazo. “Unajua jiografia ya mkoa wa Rukwa imekaa katika nyanda za juu, ni rahisi radi kulipuka maeneo haya. Hata hivyo hili suala ni la kiimani zaidi,” anasema pamoja na mambo mengi yanayosemwa kuhusu mkoa huo, kwa sasa maendeleo yanakwenda kwa kasi na anaamini miaka michache ijayo, imani za ushirikina zitapungua kama sio kwisha kabisa.

Wednesday, October 3, 2012

Pete Ya Harusi Inayoacha Maandishi “MARRIED” Kidoleni

Pete inayoacha maandishi  katika kidole cha mume wako kua “ameoa” imetengenezwa. Kwa hiyo hata jamaa yako akivua pete huko nje inaacha maandishi katika kidole “married”. Nadhani sasa wale wanaume “fulani” watadakwa lol..
Wanaume mtakubali kuvaa pete hii kweli??

Tuesday, October 2, 2012

BASI LA DAR EXPRESS LAWAKA MOTO SAFARINI

Photo: Habari zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema watu 65 wamenusurika kufa eneo la Segera Mkoani Tanga baada ya basi la Dar Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar Es Salaam kuteketezwa na Moto.

Picha kwa Hisani ya Jamii ForumsHabari zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema watu 65 wamenusurika kufa eneo la Segera Mkoani Tanga baada ya basi la Dar Express lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar Es Salaam kuteketezwa na Moto.

Monday, October 1, 2012

SOMO HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE


.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

MAONYESHO YA TIGO CIRCUS MAMA AFRICA YAENDELEA KUTIKISA JIJI LA DAR.

Walimbwende wa kundi la Tigo Circus Mama Africa wakitoa burudani wakati wa maonyesho hayo yanayoendelea katika ukumbi wa Mancom Centre uliopo New World Cinema Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Sarakasi za aina yake na michezo ya aina yake.
Steve R & B wa Kundi la InAfrika Band (Kulia)  sambamba na wenzake wakitoa burudani kwenye onyesho la Tigo Circus Mama Africa linaloendelea jijini Dar.
Watoto wa Mataifa mbalimbali wakionekana kuvutiwa na kunogewa wakati wa maonyesho ya Tigo Circus Mama Africa yanayoendelea katika ukumbi Mancom Centre uliopo New World Cinema Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Vicheko na furaha vilitawala kutoka kwa wakubwa na wadogo.
 Kundi la Circus Mama Africa wakionyesha umahiri wao wa kupiga Sarakasi kwenye mambo ya chuma.
 Pichani Juu na Chini ni Michezo Mbalimbali ikiendelea kuonyeshwa mwisho mwa wiki hii katika Ukumbi wa Mancom Centre uliopo New World Cinema Mwenge jijini Dar es Salaam.
 Mashabiki nao waliingia kwenye Stage na kupagawisha kwa kuonyesha vipaji vyao kama wanavyoonekana pichani.
Mmoja wa watoto akijaribu kuiga yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo huku akicha wazazi hawana mbavu.
Shoo ya aina yake ikiendelea.
Msanii Bongo Mtshali kutoka Afrika Kusini.
 Waka waka eeeehhhh…!!! Huyu binti kutoka Afrika Kusini ana kipaji, hebu tembelea pande zile basi usingoje kuona picha tu, kashuhudie kwa macho yako.
In Afrika Band nao wakipita mbele ya mashabiki kutoa shukrani kwa mahudhurio yao.
 Kundi la Tigo Circus Mama Africa wakito shukrani kwa mashabiki waliohudhuria Onyesho hilo.
Pichani Juu na Chini ni Umati wa Wazazi na Familia zao walioshuhudia Onyesho la Tigo Circus Mama Africa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mancom Entertainment Bw. Costantine Magavilla akiwa na MC wa Onyesho la  Tigo Circus Mama Africa.
Wazazi leteni watoto wenu kushuhudia Onyesho la Tigo Circus Mama Africa yanayoendelea katika ukumbi wa Mancom Centre uliopo New World Cinema jijini Dar es Salaam