Tuesday, September 4, 2012

ALICHOSEMA CRISTIANO RONARDO BAADA YA KUULIzWA KWA NINI HAKUSHANGILIA ALIPOFUNGA MAGOLI MAWILI


0

.
Nafahamu watu wengi wamejiuliza sana kwa nini Christiano Ronaldo alifunga magoli mawili juzi kwenye mechi na kwenye mechi na Granada lakini hakushangilia hata kidogo kitu ambacho sio kawaida yake.
Stori ni kwamba Ronaldo amekubali kutoa sentensi yenye maneno machache kuhusu yeye kutokushangilia ambapo Kauli iliyonukuliwa na Sky sports kutoka kwa Ronaldo ni kwamba, ni kweli yuko kwenye huzuni na timu yake ya Real Madrid inafahamu chanzo cha huzuni yake ambayo ndio sababu iliyomfanya asishangilie wakati alipofunga magoli mawili kwenye ligi ndani ya mechi iliyochezwa jana dhidi ya Granada.
Ungetarajia kwamba Ronaldo angeshangilia kupitiliza juzi (september 2) kwasababu alifikisha magoli 150 kwenye mechi yake ya 149 toka ajiunge na club hiyo lakini haikua hivyo.
Cristiano ambae miezi michache iliyopita alinukuliwa akisema anapenda kuichezea Real Madrid kwenye maisha yake yote yaliyobaki kwenye soka, amesema kilichomfanya asifurahi sio ishu yake binafsi bali ni ya kikazi zaidi na hakutaka kuongeza chochote kwenye hiyo kauli.

No comments:

Post a Comment