Tuesday, September 25, 2012

Mch. Chrstopher Mtikila ashinda kesi ya kumkashfu Rais JK

Picture
Mchungaji Christopher Mtikila akifurahia ushindi baada ya kushinda kesi dhidi yake.
MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ameshinda kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili.Akizungumza baada ya kushinda kesi hiyo, Mtikila amesema, “Ushindi huu niliutarajia maana hata asubuhi kabla ya kuja mahakamani niliongea na Yesu na sasa amenijibu”. Mara baada ya kushinda kesi hiyo lilizuka timbwili lingine baada ya mtu mmoja kujitokeza akiwa na RB (Report Book) akimtuhumu Mchungaji Mtikila kuwa alimtishia kumuua na ni mwizi wa viwanja. Baada ya kutaka kukamatwa na polisi mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo, Mchungaji alikataa kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa kitaifa hivyo hawezi kukamatwa na polisi mwenye cheo cha Koplo, labda polisi mwenye cheo cha SSP (Senior Superintendent of Police). Kwa kauli hiyo polisi alishindwa kumtia nguvuni.
Taarifa via GPL
Picture
Mtikila amkimsikiliza Koplo wa Polisi mwenye RB Namba : KMR/RB/10482 yenye maelezo ya kutishia kuuwa kwa maneno na wizi wa viwanja iliyofunguliwa na bwana Gotta Ndungulu.
* “Hukumu dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, iliyoahirishwa mara mbili kwa sababu ya hakimu kuwa na dharura, ilisomwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu a Hakimu Mkazi Mfawidhi, Illivin Mugeta aliyeisikiliza kesi hiyo ya kutoa maneno ya uchochezi.Mtikila alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kusambaza waraka wa uchochezi dhidi ya Rais Jakaya Kikwete, kwamba anataka kuuangamiza Ukristo. Mshitakiwa Mtikila alifunga ushahidi kwa kuwa na mashahidi wawili wa utetezi, akihofia kupoteza fedha za Serikali kwa kuwaleta mashahidi wengi ambao hawana kitu tofauti na mashahidi wengine waliokuwa wamewasilisha ushahidi wao mahakamani hapo.
Mtikila, anadaiwa kwamba, Aprili, 2010 Dar es Salaam, alisambaza waraka aliokuwa akidai ni wa kuunusuru Ukristo wenye lengo la kuangamizwa na Jihad ya Rais Jakaya Kikwete na kwamba Wakristo wajitoe mhanga kukomesha ugaidi, “Kikwete anaangamiza Ukristo, amekuwa jasiri wa kuingiza Uislamu katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alidai Mtikila katika waraka wake huo.
Alidai waraka uliosambazwa alisaini akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kuunusuru Ukristo na walichapisha nakala 100,000, lakini aligoma kutaja mahali walipochapishia nakala hizo. Maelezo yote hayo yalitolewa mahakamani kama kielelezo na ofisa wa polisi, SSP, Ibeleze Mrema aliyemuhoji Mtikila Aprili 14, 2010.”
(* ” nukuu ya taarifa ya gazeti la MTANZANIA le leo kabla ya hukumu kusomwa)
Picture
Mtikila akiondoka Mahakamani baada ya kushinda kesi na kutokamatwa na polisi.

No comments:

Post a Comment