Msajili wa vyama vya siasa nchini
John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya
kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote
kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa
habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria
inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za
uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria
inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.
No comments:
Post a Comment