Friday, September 7, 2012

AIBU: WASANII WA FILAMU WAENDEKEZA LAANA YA KUPIGA PICHA CHAFU

MREMBO ambaye pia ni msanii wa filamu Bongo, Mary John ‘Maua’ amepiga picha za utupu, kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Kitanzania.
Baadhi ya picha hizo ambazo Ijumaa linazo, zinamuonesha mwanadada huyo akiwa mtupu sehemu ya juu ya mwili wake huku sehemu ya chini akiwa amevaa taiti tu na nyingine akiwa anatunisha matiti yake.
Akizungumza na mwandishi  wetu ,mmoja wa marafiki wa karibu wa msanii huyo alisema  Maua amekuwa na tabia hiyo ya kupiga picha chafu kwa muda mrefu na hata matiti yake ametumia dawa za Kichina.
“Yule mbona anazo picha nyingi za utupu, unashangaa hizo, kuna nyingine ni mbaya kabisa,” alisema mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Katika kupekua zaidi, mwandishi wetu alimtafuta Maua na alipopatikana alikiri kuwa hizo picha ni zake.

No comments:

Post a Comment