Mmoja wa wafanyakazi wa daraja hilo ambaye jina lake halikupatikana
mara moja akiendelea na zoezi la kupiga picha huku akiwa amesimama
kwenye mtando unaopitisha umeme mwingi bila kuchukua tahadhali wakati
waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alipokua akikagua maendeleo ya
ujenzi wa daraja hilo leo. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima
kiwango cha lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya
Kajima ya Japan leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka
kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa
Japani nchini Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni
ya Kajima. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (mbele) akiwa amefuatana na
balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada, Mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam na viongozi wengine wa wizara akikagua moja ya sehemu ya barabara
ya Kilwa inayojengwa upya na kampuni ya KAJIMA ya Japan kutokana na
barabara hiyo iliyokamilika hapo awali kuwa chini ya kiwango na serikali
ya Tanzania kuikataa na kuiagiza kampuni hiyo iijenge upya kwa gharama
zake. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la
Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka
kulia) Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka
kulia) leo jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na
kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni
214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015 (Picha na Aron Msigwa –
MAELEZO)
No comments:
Post a Comment