Friday, September 21, 2012

PICHA & MAELEZO; Lema Alivotingisha Arusha Baada ya Hukumu Kuahirishwa



Msafara wa aliekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjii ukitokea mahakamani kuelekea katika ofisi za chama


Picha juu na chini wamama wakiwa wanapita njiani wakishangilia aliyekua mbunge wa arusha mjini -Chadema Mh,Godbless Lema wakati akipita kutoka mahakamani


Msafara wa aliekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini-Chadema Godbless Lema ukitokea mahakamani kuelekea katika ofisi za chama

Gari ya aliyekua mbunge wa Arusha mjini(CHADEMa)Godbless lema likiwa inasukumwa na mashabiki mara baada ya kutoka mahakamani

Aliyekua Mbunge wa arusha mjini(CHADEMA)Mh Godbless Lema akiongea a wananchi nje ya ofisi ya chama mara baada ya kutoka mahakamani leo


wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza aliyekua mbunge wa arusha mjini-Chadema Mh Godbless lema

Hawa ni makamanda waliokuwa wamevalia Tisheti za M4C huku mungine akiwa ameshona kanzu kabisa

Gari ya polisi ikiwa inapisha maandamano yapite
—-
RUFAA ya kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), ambao ulikua inatarajiwa kusikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande na wenzake, Natalia Kimaro na Salum Massatiumesikilizwa ila kesi imearishwa.
Kesi hiyo ambayo ilikuwa inatolewa maamuzi jana imeairishwa na jaji mkuu wa Tanzania kwa kile kilichodaiwa kuwa wakili wa upande wa mkata rufaa na wakili wa serekali kupata matatizo ya kufiwa na baba yao mzazi
Jaji mkuu alifikia hatua ya kuamua kesi hiyo ihairishwe hadi pale ifikapo October 2 mwaka huu ambapo ndipo imesemekana huku ya kesi hiyo ndio itakapo tolewa.
Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ambapo aliyekuwa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alongea na wananchi walikuwa wakimsindikiza nae aliwasihi wananchi hao kuwaombea majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki.
“mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi”alisema lema
Alibainisha kuwa mbali na kuzindua kampeni pia wanampango wa kuzindua mikutano ambayo itajulikana kufa au kupona ,mkutano ambao utafanywa nyumba kwa nyumba pamoja na kitongoji kwa kitongoji

No comments:

Post a Comment