Thursday, September 6, 2012

ALICHOSEMA PRODUCER MANECK BAADA YA KUONA DOGO JANJA ANATAKA KUMGOMBANISHA NA MARCO CHALI.

.
Producer Maneck ambae ni mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012 ameamua kuzungumza ya moyoni kwa kuijibu kauli Dogo Janja aliyoitoa kwamba Producer huyo kauponda uwezo wa Marco Chali.
Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar es salaam jumapili iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu ya V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na kumpiga biti kwamba asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja akashuka chini kwenda kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae ni Ustaz Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja na PNC waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni ilikua irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida sana kwa sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya kusikia kwamba Dogo Janja amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri akisema “ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo, Marco Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri, siwezi kuongea kitu kibaya kwa Marco kwa sababu leo na kesho nitamfata nitamuomba msaada wa kitu chochote kile hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano sasa, Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani ataacha hizo tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa mbali sitaki uongee na mimi that’s all”

No comments:

Post a Comment