Sunday, September 23, 2012

"NIKITAKA KUOA NITAFANYA MCHUJO KAMA WA BONGO STAR SEARCH"...HII NI KAULI YA HEMEDI ILIYOLAANIWA VIKALI NA JACK WA CHUZ





Baada ya msanii wa filamu bongo Hemed Suleiman ‘P.H.D’, kutangaza endapo akiamua kuoa basi atafanya mchakato kama wa BSS au mashindano mengine ili kufanya mchunjo wa mwanamke mzuri atakayekuwa mke wake, Jackline PantezelJack wa Chuz, amedai kuwa kitendo alichokisema msanii huyo kinahitaji awaombe msamaha wanawake kwani anawafananisha na samaki wanaovuliwa kirahisi.
 
Kauli ya Jack inaonesha wazi kuwa anawatetea wanawake na hataki waonekane kama hawana maana yoyote ndani ya jamii au watu wanaokaa na kusubiri kuolewa tu wakati maisha ya sasa hayapo hivyo, na mwanamke yeyote atakaejitokeza kwenye mchakato huo atakuwa hana akili na atakuwa ni kahaba.


“Nilisikia tu kwamba anataka kufanya kitu kama BSS katika kutafuta mwanamke wa kuoa, na hapo ina maana kuwa tayari amesha wafanya wanawake kama samaki.

Nailaan  sana  kauli hii  na ni bora  Hemed  atuombe  Msamaha” alidai Pentzel

No comments:

Post a Comment