Monday, September 10, 2012

TRENI ZA ABIRIA DAR ZAFANYIWA MAJARIBIO LEO. Kuanza rasmi mwezi wa 10



Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza,yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa  Safari zitazoanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi,majaribia hayo
yameongozwa asubuhi ya leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba(Mb) ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya
ukarabati wa njia,injini na mabehewa.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRL)wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo abubuhi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(Mb) dirisha la pili kutoka kulia,akiangalia nje wakati wa majaribio ya mabehewa sita kati ya kumi na mbili yatakayofanya safari zake kutoka Station mpaka Ubungo kuanzia mwezi wa Kumi mwaka huu,Treni hizo zitasaidia wananchi katika usafiri jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment