KUWA wazi kwa mwenzi wako ni mojawapo ya mambo ya msingi sana katika kuimarisha uhusiano. Kilicho cha msingi ni kuwa makini na namna ambavyo unazungumza na mwenzi wako.
Wakati mwingine kama unashindwa kujua namna ya kuzungumza, mnaweza kujikuta mnaanisha ugomvi badala ya kuelewana.
Ni kwamba wapenzi wanapaswa kusomana na kujuana kwa kina kwamba mwenzangu ana tabia gani na nini nifanye tuweze kwenda vizuri.
Kuna msomaji anauliza hivi ni kwa nini katika mahusiano mengi, kwa mfano kwenye ndoa walio wengi hawawezi kuwaambia wenza wao kuwa hawaridhishwi?
Matokeo yake wanatoka na kwenda kutafuta mahawara nje au kusaka watu wengine, je kuna ugumu gani wa kumwambia ukweli mwenzi wako au kumfundisha unavyotaka?
Jibu lake ni rahisi kwamba wakati mwingine unaweza kuchukua hatua hii ya kuzungumza mara nyingi uwezavyo, ila wapo wengine ni wagumu kukubaliana na kile ambacho unawaambia.
Ukweli ni kwamba uhusiano hujengwa kwa hekima na kuimarishwa kwa busara.
KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO.NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE.
Ndivyo ilivyo katika uhusiano kuwa msingi wa uhusiano kuwa mzuri ni kwa watu wenyewe kupata muda wa kuzungumza shida zinazowasumbua katika uhusiano wao.
Lakini pia ni suala la msingi kama ni ugonjwa, wanandoa watibiwe haraka ili kuacha kutiana kero katika ndoa, hasa kama ugonjwa wenyewe ni wenye kutibika.
Kwa mfano wakati mwingine unaweza kuona labda mwanamke mumewe anapomuhitaji, ndio anaanza kusema aaah naumwa ooh.
Wakati mwingine kama unaumwa kweli ni vizuri kusema mapema, sio hadi jamaa aonyeshe nia ya kuhitaji huduma fulani kwako. Kitendo kama hiki kinakwaza.
Kama ni mwanaume, ni vizuri kuhakikisha unakuwa imara�ni muhimu kujua kuwa wanawake wanachohitaji kwa wanaume siyo fedha wala mali zaidi, bali raha ya kweli toka moyoni.
Ni kosa kubwa ni kuhatarisha maisha ya ndoa, kwa mwanaume kutochukua hatua anapokuwa anaumwa magonjwa yanayotibika.
Ni hatari zaidi kwa mwanaume kulalamikiwa na mkewe kwamba hana nguvu za kiume. Hiyo ni dalili mbaya mno, chukua hatua za haraka; kama ambavyo kwenye matoleo kadhaa ya nyuma nilivyotaja mchanganyiko wa vyakula ambao mwanaume anaweza kula kupona kabisa tatizo hilo.
Hakuna sababu ya kulalamika unapokuwa na tatizo, bali chukua hatua.
Ingawa wengine wanaamua kutoka nje kwa sababu ya tamaa, lakini kwa asilimia kubwa kunakuwa na sababu za msingi.
Sidhani kama sababu ya kutoka nje ni kuridhishana pekee…hata kama ukimridhisha kiasi gani na haya mambo huwa ni tamaa.
Kama mtu anapenda machungwa sio kwamba hawezi kula embe na akila embe sio kwamba hataki tena chungwa. Ni lazima katika maisha kuwa na uchaguzi sahihi, kisha simama katika uchaguzi huo.
Sio mara zote kumuacha huyu na kwenda kwa mwingine ni kosa la mwenza wake, mara nyingi ni tabia ya mtu; nani ambaye hana kosa? Watu husameheana; Kwa sababu wakishaoana wanaacha kuwa wapenzi, wanakuwa watu wa ndoa!
Wengi wanashindwa kumfundisha mumewe au mkewe jinsi anavyotaka aridhishwe kwa kudhani kuwa atamuona mhuni, anahisi atamuuliza yeye kavijulia wapi hivyo.
Lakini pia wengine wanakataa hata ukimfundisha.
Ila iendelee kufahamika kuwa kutokuridhishwa ni sehemu tu ya sababu, zaidi ni tabia ya mtu, kuwa mbali na mwenzi wako, tamaa ya mali hasa pesa au kupata upendeleo katika jambo fulani (mfano kazi, cheo, madaraka n.k), kuendekeza tamaa za mwili (kuna mtu anadhani bila ngono hawezi kuishi).
Ukweli ni kwamba chanzo cha kuacha huyu na kwenda kwa yule huwa ni tamaa, mfano unakuta mwanaume ana mke mnene na anapata kila kitu anachokihitaji, lakini katika pitapita zake akikutana na mwanamke mwembamba anatamani aonje ili ajue inakuwaje ukiwa na mwembamba.
Kwa ujumla tamaa ndiyo msingi wa walio wengi kuacha huyu na kusaka mwingine.
Lakini pia ndiyo nasema inabidi kuwa makini unapomshauri mtu�uanze tu kumwambia mwanaume wa mikoa mingine…�ehhh murrrahh hauniridhishi kabisa mume wangu…..nini kitafutia?� Jibu unalo.
No comments:
Post a Comment