Walimbwende wa kundi la Tigo
Circus Mama Africa wakitoa burudani wakati wa maonyesho hayo
yanayoendelea katika ukumbi wa Mancom Centre uliopo New World Cinema
Mwenge jijini Dar es Salaam.
Sarakasi za aina yake na michezo ya aina yake.
Steve R & B wa Kundi la
InAfrika Band (Kulia) sambamba na wenzake wakitoa burudani kwenye
onyesho la Tigo Circus Mama Africa linaloendelea jijini Dar.
Watoto wa Mataifa mbalimbali
wakionekana kuvutiwa na kunogewa wakati wa maonyesho ya Tigo Circus Mama
Africa yanayoendelea katika ukumbi Mancom Centre uliopo New World
Cinema Mwenge jijini Dar es Salaam.
Vicheko na furaha vilitawala kutoka kwa wakubwa na wadogo.
Kundi la Circus Mama Africa wakionyesha umahiri wao wa kupiga Sarakasi kwenye mambo ya chuma.
Pichani Juu na Chini ni
Michezo Mbalimbali ikiendelea kuonyeshwa mwisho mwa wiki hii katika
Ukumbi wa Mancom Centre uliopo New World Cinema Mwenge jijini Dar es
Salaam.
Mashabiki nao waliingia kwenye Stage na kupagawisha kwa kuonyesha vipaji vyao kama wanavyoonekana pichani.
Mmoja wa watoto akijaribu kuiga yaliyokuwa yakijiri ukumbini hapo huku akicha wazazi hawana mbavu.
Shoo ya aina yake ikiendelea.
Msanii Bongo Mtshali kutoka Afrika Kusini.
Waka waka eeeehhhh…!!! Huyu
binti kutoka Afrika Kusini ana kipaji, hebu tembelea pande zile basi
usingoje kuona picha tu, kashuhudie kwa macho yako.
In Afrika Band nao wakipita mbele ya mashabiki kutoa shukrani kwa mahudhurio yao.
Kundi la Tigo Circus Mama Africa wakito shukrani kwa mashabiki waliohudhuria Onyesho hilo.
Pichani Juu na Chini ni Umati wa Wazazi na Familia zao walioshuhudia Onyesho la Tigo Circus Mama Africa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mancom Entertainment Bw. Costantine Magavilla akiwa na MC wa Onyesho la Tigo Circus Mama Africa.
Wazazi leteni watoto wenu
kushuhudia Onyesho la Tigo Circus Mama Africa yanayoendelea katika
ukumbi wa Mancom Centre uliopo New World Cinema jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment